Aina ya Kachumbali ya Mbichi | Huliwa Mbichi

1 Like 1 Comment

Hii ni aina ya kachumbali ambayo huliwa mbichi kabisa. Na katika vilivyomo ni kimoja tu ambacho najua kwa wengi hamjazoea kula kikiwa kibichi nacho ni Bamia.

MAHITAJI

  • Mchicha – katakata
  • Hoho – Katakata upendavyo
  • Embe dodo – menya na katakata
  • Bamia mbichi – Kataka kata slices
  • Maji ya Limao – Kijiko 1 cha mezani
  • Karoti – Katakata vile upendavyo
  • Chumvi kwa kiasi upendavyo
  • Pilipili – Kiasi upendacho (Hiyari)
  • Mafuta ya Olive Kijiko 1 cha chai ( Hiyari)

Changanya vyote katika bakuli moja; Kisha pakua katika sahani na hapo ni tayari kwa kuliwa. Kama huwezi kula bamia mbichi basi changanya na embe lililo iva na utaweza.

You might like

About the Author: Chef Kile

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *