Desert ya NDIZI MBIVU, MAZIWA FRESH, CHOCOLATE NA MKATE

4 Likes Comment

Pishi hili ni moja ya yale mapishi ambayo huwa napika kutokana na utashi wangu tu katika ubunifu. Kwa vile matokeo yalikuwa mazuri sana naona ni vema kushare nawengine wajifunze pia

MAHITAJI

  • Ndizi mbivu 2
  • Maziwa nusu glasi
  • Chocolate bar 4
  • Mkate vipande 4

KUANDAA

  1. MKATE – Toast mkate wako kisha kata katika vipande kwa shape upendayo
  2. NDIZI MBIVU – Kata vipande vidogo vigodo kisha zirosti kwa mafuta hadi ziwe rangi ya kahawia kisha kausha na wacha zipoe
  3. CHOCOLATE na MAZIWA – Yeyusha chocolate yako ukichanganya na maziwa ya uvugu vugu
  4. Vikiwa vimeyeyuka weka zile ndizi na endelea kusaga saga hadi vilainike kwa pamoja vyote.
  5. Sasa anza kupaka mkate wa kwanza chini, kisha weka kwa sahani kila layer unaiwekea huo uji wa chocolate , maziwa na ndizi hadi mwisho
  6. kisha weka kwa friji ipoe kidogo na tayari kwa kula.

Ni rahisi na ni tamu sana

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *