Jinsi Kupika Kabichi Kwa Tui la Karanga

2 Likes Comment

Sasa wengine wanaita hii kabichi na wengine wanaita kabeji ; yote sawa kwa vile inatokana na jila la Kiingereza Cabbage.

Hapa nakuonyesha namna ya kuipika kabichi na karanga. Mimi nakumbuka tangu udogoni mboga hii ilikuwa ikipikwa na bibi au mama wakati mwingine. Kusema kweli huwa ni tamu sana. Karanga ambazo hutumika ni vema kama zikiwa zimekaangwa kidogo kabla ya kuzisaga. Lakini pia hata karanga ambazo husagwa bila kukaangwa zinafaaa tofauti inakuja kwenye muda wa kukaa jikoni.

Ila kwa sisi wa mjini sikuhizi tunatumia hizi Peanut Butter kurahisisha mambo.

MAHITAJI

 • Kabichi 1/2 icharangwe /katakata
 • Punje 2 za kitunguu swaumu – ponda ponda
 • Vijiko 4 vya siagi ya karanga ( Peanut Butter)
 • Vitunguu maji 2 katakata
 • Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya mezani
 • Kiasi cha chumvi upendavyo
 • Pilipili ( Hiyari)
 • Viungo majani – kama giligilani, rosemary , oregano n.k waweza weka ila ni hiyari
 • Karoti 1 – Katakata vile upendavyo

JINSI YA KUPIKA

 • Weka sufuria yako kwa moto wa kati; weka mafuta yakisha pata moto kiasi weka vitunguu maji na uvikaange kwa dakika kama 2 ; Kisha weka kile kitunguu swaumu endelea kukaanga hadi vitakapoanza kuwa na rangi.
 • Sasa hapo weka maji kidogo kama kikombe kimoja¬† na uweke na siagi ya karanga. Hapa wakati waendelea kukoroga ukiona uji unakuwa mzito ongeza maji hadi upate uji mwepesi kiasi. Kisha acha uchemke kwa dakika 3 – 4 kwa moto mdogo.
 • Sasa weka ila Kabichi yako katika huo uji na endelea kukoroga huku vikichemka kwa pamoja kwa dakika chache hadi kabichi ilainike kabisa – Pia weka chumvi wakati huo.
 • Ikiisha kulainika unaweza ongeza karoti ,pilipili , viungo majani na kuacha vinaiviana katika moto mdogo kwa dakika chache tu.
 • Baada ya hapo mboga ipo tayari kwa kuliwa na ugali ama wali inafaa zaidi.

Mpangilio huu wa mapishi kwa kutumia karanga unaweza kuutumia katika Kisamvu, spinach, mchicha na mapishi yakatoka matamu tu.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *