Jinsi Kupika Pilau la Kiswahili Kwa Tui la Nazi

11 Likes Comment

Karibuni tena. Yaani mimi jamani huwa pilau langu lazima niweke nazi na huwa linanoga sana. Sasa nimegundua wapinshi wengi huwa hawautumii nazi. Hivyo basi nikaona ni vema niwaonyeshe namna sahihi ya kupika pilau na vilevile kulipika pilau la nazi. Pia nimeweka na video yangu nikipika ivo waweza jifunza zaidi.

MAHITAJI

 • Mchele 1/2 kg – Ondoa mawe na kupepeta ila usioshe mchele
 • Vitunguu maji 2 – katakata
 • Vitunguu swaumu – punje 4 – katakata au twanga
 • Nyanya moja – Katakata
 • Nyama – 1/2 kg
 • Chumvi kiasi upendacho
 • Mafuta ya kula vijiko 4 vya mezani
 • Tui La Nazi
 • Pilau Masala vijiko 2 vya mezani
 • Mahanjumati masala kijiko 1 cha mezani (Hiyari ila ni nzuri sana kama unayo)

JINSI YA KUPIKA PILAU LENYEWE

 1. Kwanza kabisa chemsha nyama, hapa unaweka chumvi kidogo na vitunguu swaumu punje mbili tatu hivi. Wacha nyama ichemke hadi kuiva. Hakikisha unakuwa na supu ya kutosha ili itumike kupika pilau. Hivyo unaweza ongeza maji katika kuchemsha nyama.
 2. Nyama ikiwa tayari weka sufulia husika katika moto na uweke mafuta ya kula, yakipata moto kiasi weka vitunguu maji. Vipike kwa dakika 2 kisha weka vitunguu swaumu endelea kwa sekunde chache kisha weka ile nyanya moja.
 3. Endelea kuipika nyanya hadi iwe kama inapotea hivi ndipo unaweka nyama zote ila bila mchuzi. Kaanga pamoja kwa dakika moja tu kisha unaweka ule mchuzi wa nyama na viungo vya pilau na ile mahanjumati masala pamoja na chumvi kiasi upendacho. Koroga kwa dakika moja hadi vianze kuchemka pamoja.
 4. Sasa weka mchele na lile tui la nazi kurogoga kwa sekunde kama 3o hivi. Kisha punguza moto na funika kwa dakika 10 kisha angalia na kugeuza
 5. Baada ya kugeuza angalia kama unahitaji maji waweza ongeza maji ya vuguvugu kiasi pia kama unahitaji kupalilia huo ndio muda, wengine huweka katika oven; fanya kwa jinsi mazingira yanakuruhusu. Ila ni kwa dakika zingine 10 na pilau litakuwa tayari kwa kuliwa.

MUDA KAMILI ITACHUKUA KUIVA KWA PILAU INATEGEMEA NA WINGI WA PILAU

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *