Jinsi ya Kuchoma Kiazi Kwenye Microwave

1 Like Comment

 

Kuna mapishi mengine huwa ni ya haraka sana. Hapa nakushikirisha namna ya kumicrowave kiazi na hii hufaa sana kuwa kitafunwa katika stafutahi mida ya asubuhi.

Kwa watu 2

MAHITAJI

  • Viazi mviringo 2 vikubwa ( usimenye ila vioshe vizuri)
  • Asali vijiko viwili vya mezani

JINSI YA KUPIKA

  1. Chukua viazi na uvichome chome kwa kutumia uma vile vitobo vitasaidia kuivisha had ndani; weka katika sahani au chombo kinachofaa katika microwave – Weka na set dakika 10. Ikifika daki 8 au 9 angalia na kama tayari toa au wacha vimalize zile dakika 10 kama bado.
  2. Vikiwa tayari vitoe na upasue katikati na unyunyuzie asali na hapo vinakuwa tayari kwa kuliwa.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *