Jinsi Ya Kuchoma Nyama Kitaalam | Nyama Choma

12 Likes Comment

Mimi ni mmoja kati ya wachoma nyama wazuri sana katika tasnia hii ya mapishi. Sasa naona ni vema nikashirikiana nanyi wapenzi wa mapishi na wale wapenzi wa nyama juu ya uchomaji sahihi wa nyama. Hivyo hii leo sio kama recipe ila ni kufundishana.

Nyama ambayo leo itatumika hapa ni ya Ng’ombe. Siku nyingine nitawaandikieni juu ya nyama zingine.

Uchomaji wa nyama una namna nyingi sana kuanzia maandalizi kwa maana ya marination hadi kuchoma nyama na waichoma kwa muda gani.

Kama umekuwa unakula nyama choma na inakuwa ngumu na kavu basi ujue hao wachomaji kuna vitu wanakosea katika uchomaji. Na kwa vile leo somo lipo juu ya nyama ya Ng’ombe basi tuendelee.

Ikiwa wewe ni mchomaji na unataka kuwa unapata nyama bora basi ni vema ukafuatilia tangu Ng’ombe hajachinjwa na ujue uzito wake.

VITU VYA KUZINGATIA:-

  • Nyama nzuri ya kuchoma inatakiwa Ng’ombe asiwe na uzito unaozidi kilo 110.
  • Nyama nzuri ni ile iliyolala au kuachwa kwa muda mrefu ikining’inia na kuchuja maji yote
  • Nyama nzuri ya kuchoma ni Sehemu za Mbavu na Kidari,
  • Nyama nzuri ya kuchoma lazima iwe na mafuta asili ya mnyama mwenyewe

VIUNGO

Katika uchomaji wa nyama unahitaji chumvi tu kama kiungo pekee na kimsingi kinatosha. Ila kwa sasa unaweza ongeza hapo pilipili manga, mustard, paprika, rosemary, cayenne spices na vingine kadiri upendavyo.

SWALA MUDA KATIKA UCHOMAJI WA NYAMA

Hili naweza kuliweka katika mafungu mawili. Kuna zile ambazo ndani ya dakika 20 zinakuwa tayari kwa kuliwa  na kuna ambazo huchomwa si chini ya masaa 4 hadi 24 kufikia kiwango cha kukubarika.

Nyama nzuri ya kuchoma ukitaka kuipata ikiwa laini basi ni vema iwe haijaivaa kwa asilimia 100, ila iwe imeiva asilimia 50 na kuachwa kupumzika kwa dakika 10 baada ya kutoka katika moto na kuwa served. Utaratibu huu ni kwa zile zinazochomwa kwa dakika chache.

Zile nyama zinazoiva kwa masaa mengi zinatakiwa kuiva kwa asiliamia 100 lakini zibaki na supu nzuri. Hivyo uchomaji wake ni ule wa joto la mbali na sio karibu. Moto mdogo na kuiva kwa muda mrefu.

Nyama hii ya sehemu ya Mbavu za Ng’ombe iliiva kwa masaa 7 katika joto la mbali

 

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *