Jinsi ya Kupika Burger ya Yai | Baga la Yai

9 Likes Comment

Najua wengi mmezoea Burger za nyama ila hata za mayai zipo na ni tamu sana. Sasa ndio ivo wajua Burger asili yake sio Afrika na ivo hatuna jina la kiswahili ivo twaweza ila tu Baga. Hapa ntakuelekeza jinsi ya kuipika na pia utaona kwa njia ya video kutoka kwenye YouTube Channel yangu.

MAHITAJI

 • Mkate wa Burger / Baga 1
 • Nyanya slice 2
 • Kitunguu maji slice 2
 • Yai moja
 • Tomato Sauce vijiko 2 vya mezani
 • Mafuta ya Kupikia kijiko 1 cha mezani
 • Jibini / Cheese slice moja ( Cheese ile ya Cheddar ni nzuri)
 • Mchanganyiko wa pilipili manga na chumvi – 1/2 cha chai

JINSI YA KUPIKA BAGA

 1. Kwanza kata ule mkate wa baga kwa kuugawa mara mbili nusu kwa nusu kwa ubapa.
 2. Weka pan katika moto kisha wacha ipate mote kidogo. Waitumia kukausha kidogo mikate yako kisha waiweka pembeni.
 3. Sasa weka mafuta katika hicho chombo alafu weka yai moja bila kulikoroga – Ndio ile tunaita yai la jicho la Ng’ombe. Kisha nyunyiza ule mchanganyiko wa chumvi na pilipili manga sasa kiasi gani unapenda yai lako liive ni uamuzi wako. Mimi huwa siligeuzi kabisa ivo naivisha upande moja mda mrefu.
 4. Yai likiwa motoni weka kipande cha cheese / jibini sasa wakati inayeyuka
 5. Pakaa tomato sauce kati mkate ule wa chini kisha weka slice ya kitunguu na nyanya na sasa epua lile yai na kuweka juu yake, sasa unaweza ongeza tomato sauce na kumalizia zile slice za nyanya na kitunguu na kuweka mkate wa juu.
 6. Hapo Burger yako ipo tayari kwa kuliwa.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *