Jinsi ya Kupika Mboga Mnafu na Siagi ya Karanga

2 Likes Comment

Mboga hii maarufu sana hapa kwetu; mbali na kuonekana ni mboga ya kawaida sana ila kusema kweli inavirutubisho vizuri sana ambavyo tunavihitaji. Mimi huwa naipika hii kwa namna ambayo niliona bibi yangu alikuwa akipiga. Nakumbuka mapishi mengi ya mboga mboga , kama majani ya maboga, kabechi n.k bibi alitumia karanga. Nami hapa nimetumia karanga katika kuupika huu mnafu mtamu sana.

MAHITAJI

 • Mnafu fungu moja ( chambua na kuikatakata)
 • Punje mbili za Kitunguu swaumu – vikatekate
 • Kitunguu Maji kimoja
 • Peanut Butter vijiko 2
 • Chumvi kama upendavyo
 • Pilipili Kama unapenda

JINSI YA KUPIKA

 1. Anza kwaa kuunga kitunguu maji na garlic kwa dakika chache – Kisha weka maji kidogo yakianza kuchemka weka Peanut butter
 2. Endelea kukoroga hadi ilainike na kuwa nzuri katika uzito uupendao – mimi napenda nzito kidogo
 3. Ikifikia poa ndipo unaweka ile mboga yako na kuvichanganya vizuri kama inakuwa nzito sana ongeza maji kidogo
 4. Weka pilipili kama unapenda
 5. Sasa ni mda gani itachemka hapo ni juu ya mpishi vile unapendelea kupika mboga yako. Binafsi huwa nazima kabisa jiko na kuivisha mboga majani na joto tu kwa dakika chache kisha nakula.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *