Jinsi ya Kupika Mkate wa Ki-Irish

1 Like Comment

 

Sasa jinsi ya kupika rahisi sana haina kuumua wala kuukanda sana.

Mkate wa kula watu 3

MAHITAJI

 • Unga wa ngano 1/2kg
 • Sukari nusu vijiko 3
 • Unsalted Butter vijiko 4 ( Siagi ile ya butter)
 • Chumvi kijiko kimoja cha chai
 • Magadi Soda kijiko 1 cha chai
 • Yai moja
 • Butter Milk vikombe viwili.
 • Zabibu kavu nusu kikombe

JINSI YA KUPIKA

 1. Changanya unga, magadi soda, butter , sukari, chumvi… Vikisha changanyika weka butter milk ikiwa imechanganyika na lile yai moja kisha weka zile zabibu kavu. Kanda kanda kidogo. Huwa unga ni mlaini tu ivo usiufanye mgumu sana.
 2. Weka unga wako katika shape uipendayo
 3. Kisha weka katika oven yako kwa dakika 30 – 40 kutegemea na kiasi cha joto; Nyuzi joto ni kukadiria kutokana na jiko unalotumia

Baada ya hapo mkate upo tayari kwa kuliwa na kufurahia.
*Note* Ndio hauhitaji amira kupika mkate huu

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *