Jinsi ya Kupika Mkate wa Ndizi Mbivu

4 Likes Comment

Yaani kama wewe ni mpenzi wa mikate basi ukiutengeneza mkate huu wa ndizi mbivu utafurahi sana na wengine katika familia yako watafurahi. Na ni mkate mzuri. Ni mkate mrahisi na hauna ugumu katika kuuandaa. Leo nakupa namna ya kuupika.

MAHITAJI

 • Unga wa Ngano 1/2 kg
 • Baking Powder Kijiko 1 cha chai
 • Baking Soda Kijiko 1 cha chai
 • Siagi ya Butter 1/4 ikiwa
 • Mayai 2
 • Ndizi mbivu 3 kubwa
 • Sukari 1/4 kg
 • Chumvi kijiko 1 cha chai

JINSI YA KUANDAA NA KUUPIKA

 1. Kwanza changanya Siagi ya butter na sukari hadi vichanganyike vema kabisa
 2. Sasa ongeza ndizi kwa kuziponda ponda hadi zichanganyike vizuri kabisa
 3. Ongeza yale mayai 2 na endelea kuchanganya huo uji…
 4. Pasha oven yako moto kufikia nyuzi joto 180
 5. Sasa ni unga – ( unga uwe ushaweka baking powder , baking soda na chumvi) . Sasa changanya unga wako na mchanyiko mwingine upate uzito wa kati ila sio ngumu sana. Uwe mlaini laini.
 6. Andaa vifaa vya kuoka mikate vipakae mafuta ya butter kisha mimina mchanganyiko wako kwa kiasi upendacho
 7. Weka katika oven kwa dakika 55 hadi 60 … Angalia mkate wako kwa kuchomeka kisu au kijiti cha mshikaki ikiwa kitatoka bila kuwa na vitu kunatia basi mkate upo tayari. Toa na uache upoe tayari kwa kuliwa

Tazama video hii hapa chini nikionyesha jinsi ya kupika mkate huo katika Youtube.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *