Jinsi ya Kupika Ndizi Mbichi Zilizikaangwa na Njegere Ya Nazi

6 Likes Comment

Kuna baadhi ya mapishi huwa ni ubunifu zaidi kuliko recipe; Leo nakuonyesha pishi ambalo hata jina lake bado sijalipata ila soon nitakuwa na jina lake. Pishi hili linahusisha ndizi mbichi zilizo kaangwa alafu zikatumika katika sosi yenye njegere , karoti, vitunguu maji na swaumu pamoja na tui la nazi. Pishi hili zuri sana na lina ladha ya kipekee kabisa. Fata maelekezo na ujifunze.

MAHITAJI

 • Ndizi mbichi 2 – Menya kata slices
 • Njegere Mbichi – Mkono mmoja ( zinazo jaa katika kiganja chako)
 • Kitunguu maji 1 – katakata
 • Karoti 1 – kata vipande vikubwa vikubwa
 • Kitunguu swaumu punje 1 – katakata
 • Tui la Nazi kikombe kimoja ( lile tui la kwanza tu)
 • Mafuta ya Kupikia – kwa kuzikaanga ndizi
 • Mahanjumati masala kijiko 1 cha chai – Kama hauna hii waweza tumia spice mix yoyote uipendayo
 • Chumvi kiasi upendacho

JINSI YA KUPIKA

 1. Kaanga ndizi ziive na kuwa na rangi kama khahawia kwa mbali. Kisha epua weka kando
 2. Katika pan moja weka Kitunguu maji, kitunguu swaumu, karoti na mafuta ya kula kijiko kimoja cha mezani, vikaange kwa kwa dakika 2-3 kisha weka chumvi na masala uliyonayo kanda kidogo weka njegere koroga na weka maji kidogo kama vijiko vinne vya mezani. Funika kwa dakika 1-2
 3. Sasa weka tui la nazi koroga likichanganyika weka ndizi na endelea kukoroga kwa dakika 1 ; kisha pakua katika bakuli ni tayari kwa kula

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *