Jinsi ya Kupika Ndizi na Maziwa | Ndizi na Nyama

7 Likes Comment

Ushawahi kula ndizi maziwa wewe? Basi nikwambie tu ni moja ya vyakula makini sana. Na kama ukapika basi walaji watafurahia sana mlo huu wa ndizi maziwa na nyama. Hapa katika maelezo nimetumia ndizi mzuzu mbichi; ni kwa vile mimi ni mpenzi wa ndizi mzuzu. Lakini waweza tumia ndizi aina ingine kama vile mshale, matoke au mnyenyele.

MAHITAJI

 • Ndizi mzuzu mbichi 6 Menya na uzikate vipande vipande
 • Nyama ya Ng’ombe 1/4 kg
 • Vitunguu maji 2 Katakata
 • Punje 3 za kitunguu swaumu – katakata
 • Chill flakes ( Hiyari)
 • Karoti moja – katakata
 • Pilipili Manga – Nusu kijiko cha chai
 • Chumvi kiasi upendacho
 • Maziwa fresh 1/4 ltr
 • Viungo vya majani majani mf Rosemary, Oregano, Giligilani – weka kama kijiko 1 cha¬† chai

JINSI YA KUPIKA

 1. Chemsha kwanza nyama; hadi kuiva vizuri. Tunachemsha nyama kwanza maana ndizi huiva haraka
 2. Kisha weka ndizi na hivyo vingine isipokuwa maziwa. Chemsha ziive kabisa
 3. Kisha weka maziwa koroga huku inachemka kwa dakika 5 baada ya hapo epua na ni tayari kwa kula

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *