Jinsi Ya Kupika Ndizi Zilizochomwa Katika Supu ya Nyama Choma

2 Likes Comment

Hii ni moja ya supu au mchemsho utakao kula na ukabaki katika kumbu kumbu zako daima kwa jinsi ilivyo na ladha ya kipekee kabisa. Pishi nililibuni katika kujifunza mapishi mapya katika jamii yetu. Na kusema kweli ni rahisi sana kuandaa mara utakapokuwa na mahitaji yote.

MAHITAJI

 • Nyama ya Ng’ombe iliyonona 1/2 kg ( sehemu ya mbavu ni nzuri zaidi)
 • Ndizi Mzuzu 4
 • Chumvi
 • Pilipili manga
 • Mchanganyiko wa Kitunguu swaumu na Tangawizi kijiko 1 cha chai
 • Maji ya Limao vijiko 2 vya mezani
 • Mixed herbs kijiko 1 cha chai

JINSI YA KUPIKA

 1. Kuchoma nyama na ndizi – hadi ziive na ile hali ya kuungua ungua iwepo kidogo. Weka ndizi pembeni na nyama katakata katika vinyango.
 2. Katika chombo cha kupikia supu weka nyama na viungo vingine vyote – Ongeza maji kiasi cha nusu lita na wacha vichemke taratibu hadi uone nyama imelainika zaidi na kutengeneza supu.
 3. Katakata ndizi katika nijipande kisha weka katika hiyo supu na wacha vichemke pamoja kwa dakika tano.
 4. Baada ya hapo epua na kupakua maana supu ipo tayari. Kama ni mpenzi wa pilipili waweza tumia itanogesha zaidi.

NOTE:

Mixed Herbs – Ni mchanyanyiko wa viungo vya majani kama vile majani ya giligilani, rosemary , sage, oregano, etc

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *