Jinsi ya Kupika Pilipili ila ya Utamu na Ukali

3 Likes Comment

Je unapenda kutengeneza ile pilipili fulani nzuri inakuwa na ukali na utamu fulani hivi mzuri na kukufanya uendelee kuila ilhali kali maana kunakuwa na kale kalimao fulani. Basi recipe hii hapa chini inakufaa. Fanya kuitengeneza kisha uje unipe report.

MAHITAJI

  • Pilipili mbuzi 1/4 kg ziwe kijani
  • Nyanya zilizoiva vizuri 3
  • Clove za garlic 3
  • Chumvi vijiko 2 vya mezani
  • Mafuta ya kula vijiko 4 vya mezani
  • Maji ya limao vijiko 4

JINSI YA KUIPIKA

Blend kila kitu pamoja isipokuwa yale Maji ya malimao. Ukishablend chemsha kwa joto la wastani kwa dakika 20. Epua kisha weka Maji ya limao. Acha ipoe dakika 5 na hapo itakuwa tayari kwa matumizi.

Unaweza hifadhi kwa friji na kutumia kidogo kidogo.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *