Jinsi ya Kupika Supu kwa Kichwa cha Samaki

4 Likes Comment

 

Hapa nakuja na namna ya kutengeneza supu ya kichwa cha samaki, inaweza kuwa aina yoyote ile ya samaki. Kuna ambao huwa kichwa wanakitoa kabisa. Basi nikwambie tu katika kichwa cha samaki kuna supu nzuri sana na yenye afya tele.

Supu kwa watu 2

MAHITAJI

 • Vichwa 2 vya samaki
 • Maji ya limao 1
 • Pilipili Hoho 1 ( Pasua kati kati ondoa mbegu na uikatekate)
 • Karoti 2 ( zikatekate)
 • Chumvi kiasi utumiacho
 • Pilipili manga nusu kijiko cha chai
 • Mchanganyiko wa viungo vya mimea ( mixed herbs) kijiko 1 cha chai

JINSI YA KUIPIKA SUPU

 1. kwanza andaa vichwa vya samaki kwa kuvisafisha vema , kama wapenda unaweza ondoa hadi macho.
 2. Kisha weka katika chombo na uanze kukichemsha. Weka maji, chumvi kiasi, pilipili manga, mixed herbs na uwache vichemke kwa dakika 8 – 10 ndipo uweke karoti,pilipili hoho, maji ya limao kisha acha vichemke dakika chache huku ukiangalia kama imeiva.
  Ni hivyo tu supu inakuwa ipo tayari kwa kuliwa. Hapo nimeweka vitu vichache ila unaweza ongeza vingine zaidi kama kabichi au mboga zingine za majani nk.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *