Jinsi ya Kupika Supu ya Kuku | Supu Ya Kuku na Machungwa

3 Likes Comment

Karibuni; Leo nakupa recipe nzuri kabisa ya kupika supu ya kuku. Pishi hili ni rahisi sana na wengi twaliweza.

MAHITAJI

 • Kuku 1/2 kg – kata vipande upendavyo
 • Punje 2 za kitunguu swaumu
 • Mahanjumati masala kijiko 1 cha chai
 • Pilipili Manga 1/2 kijiko cha chai
 • Udaha / Cayenne Spices 1/4 ya kijiko cha chai
 • Viungo majani kama giligilani, rosemary , bay n.k vijani vichache
 • Pilipili Mbuzi upendavyo na ni hiyari
 • Chumvi kiasi upendacho
 • Juisi ya Chungwa moja
 • Mafuta ya kula vijiko 2 vya mezani

JINSI YA KUIPIKA SUPU YA KUKU

 1. Kitu cha kwanza ni kuzibrown zile kuku – weka pan yako katika moto na mafuta kiasi kama kijiko kimoja au viwili. Pan ikipata moto weka vile vipande vya kuku ni kama wavibabua hivi kila upande viwe na ile rangi ya khahawia au kama kuungua ungua hivi.
 2. Vikiwa tayari weka maji kama nusu lita na vitu vingine vyote isipiokuwa juisi ya chungwa. Acha vichemke katika moto wa juu kwa dakika 3 kisha punguza moto na uwache vichemke kwa dakika 10 – 15 . Au niseme hadi pale utakapoona kuku imeiva na supu yaonekana vizuri.
 3. Dakika moja kabla ya kuipua ndio unaweka ile juisi ya machungwa katika supu yako. Baada ya hapo supu iko tayari kwa kuliwa.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *