Jinsi ya Kupika Uji na Siagi ya Karanga | Peanut Butter Porridge

2 Likes Comment

Leo tupike uji wa kuweka ile siagi ya karanga kwa lugha ingine Peanut Butter; Mahitaji yake marahisi tu.

MAHITAJI

  • Unga wa dona au sembe vijiko 3 vya mezani
  • Sukari vijiko 3 vya mezani
  • Siagi ya karanga vijiko 2
  • Maji ya kwa ajili ya kupika uji Takribani 1/2 later

JINSI YA KUUPIKA

  1. Kwanza bandika maji hadi yachemke
  2. Weka unga kwenye kibakuli kisha weka maji kiasi baridi ; changanya vizuri kisha mimina kwenye maji yanayochemke hadi pale uji utakapokuwa mzito kiasi na kuendelea kuchemka. Wacha uchemke katika moto wa kati kwa dakika 5 – 7
  3. Ongeza sukari kisha koroga vema na uweke ile siagi ya karanga na uendelee kukoroga hadi vichanganyike vema. Ikiwa unakuwa mzito sana unaweza kuongeza maji ya vugu vugu kupata ulaini unaoupenda.
  4. Kisha acha tena kwa dakika 2-3 na baada ya hapo uji unakuwa tayari kwa kuliwa.

Waweza tazama hii video hapa jinsi nimeelekeza kuupika uji huu mtamu sana.

 

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *