Jinsi ya Kupika Wali Mayai | Nzuri kwa Mchana

19 Likes 3 Comments

Hili ni lile pishi la kivivu kiasi maana ni rahisi sana. Wengi hulifanya asubuhi maana wanatumia kiporo cha wali. Sio lazima iwe ni kiporo waweza pika wali kisha ukishapoa ndio wautumia katika pishi hili la leo.

MAHITAJI

  • Wali Vijiko 4 vya mezani – Uliopikwa na kupoa
  • Mayai 4
  • Chumvi kiasi upendacho
  • Karoti moja – katika kata vile upendavyo
  • Mafuta ya Kula vijiko 3 vya mezani

Ukiangalia hapo katika mahitaji kuna vitu vichache. Naam hivyo ni kwa vile nilivyopika mimi ila unaweza weka ubunifu ukaongeza vingine kama viungo, mboga mboga zingine, hata nyama ilokwisha iva, pilipili na vinginevyo.

JINSI YA KUPIKA

  1. Pasua mayai yote na uyapige pige, weka ule wali ( wali uwe umekauka vizuri na sio wa maji maji) , weka na chumvi kidogo , na viungo vingine kama unavyo. Changanya vyote upate ulaini kama uji uji.
  2. Weka mafuta katika pan unayotumia na yawe katika moto wa kati ndipo umimine mchanganyiko wako. Pika katika moto mdogo kila upande kwa dakika kadhaa hadi utakapoona rangi ya ukhahawia yatokea. Hivyo utakuwa ukigeuza mara kadhaa. Usichanganye ila geuza kama chips mayai.
  3. Baada ya hapo pakua na weka katika chombo kisha weka karoti kama kuwekea nakshi tu ( garnishing )

You might like

About the Author: Chef Kile

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *