Jinsi ya Kupika Wali wa Binzari Manjano

4 Likes 2 Comments

Habarini wapenzi wa mapishi. Leo hapa nawshirikisha katika pishi la wali wa binzari manjano. Wali huu ni mtamu sana na rangi yake ambayo huwa ni njano huwa ni nzuri sana. Pia ni rahisi sana kupika na ukishauwezea basi wakati wote utapika wali kwa namna hii nzuri.

MAHITAJI

 • Mchele 1/4 kg
 • Kitunguu swauma punje 2 katakata
 • Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya mezani,
 • chumvi kiasi upendacho
 • Binzari manjano kijiko 1 cha chai
 • Karoti moja – katakata
 • Siagi ya butter kijiko 1 cha mezani (Hiyari)
 • Mixed herbs kijiko 1 cha chai ( Hiyari )
 • Maji

JINSI YA KUUPIKA WALI HUU

 1. Weka sufuria yako katika moto na uweke mafuta yakipata moto weka vitunguu swaumu kaanga kwa sekunde chache.
 2. Weka mchele – Mimi huwa sioshi mchele ivo kama wewe waosha bado sio tatizo. Ukishaweka mchele koroga kidogo kisha weka vifuatavyo , binzari manjano, chumvi, mixed herbs kisha koroga kwa dakika moja.
 3. Sasa weka maji ( hiyari yako maji yawe ya moto au baridi) Ukishaweka maji funika vizuri kaabisa weka moto wa kati. Hivi waacha hadi pale wali utakapo iva yaweza kuwa dakika 10 – 15.
 4. Sasa unaweka zile karoti na siagi ya butter kisha wavichanganya vema katika wali. Kisha funika tena kwa dakika 3. Baada ya hapo wali ni tayari.

Hapo wali upo tayari. Waweza pakua na kurembesha kiasi.

You might like

About the Author: Chef Kile

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *