Jinsi ya kutengeneza Biskuti Kwa vitu Vitatu Tu

8 Likes Comment

 

Naam leo nakuonyesha njia rahisi sana ya kutengeneza biskuti nzuri na tamu sana kwa kutumia mahitaji matatu tu. Ni pishi rahisi sana na waweza kutumia jiko la oven au jiko la mkaa wa kawaida.

MAHITAJI

  • Mafuta ya Butter au Blue Band kiasi ya robo kg
  • Sukari ile laini robo
  • Na Unga (All purpose flour)

NAMNA YA KUANDAA NA KUOKA BISKUTI

  1. Kwanza changanya butter/blueband na sukari – vichanganye hadi vilaini kabisaaa, kisha ongeza unga wa baking hapo pia changanya sana vya kutosha hadi unga uwe washikana – kumbuka mahitaji ni hayo matatu usiongeze maji.
  2. Baada ya kuwa umeuchanganya vema unga wako uhifadhi kwa friji au mahali tulivu kwa dakika 20 hivi. Pasha jiko lako moto kama watumia oven au kama ni mkaa uwe tayari.
  3. Baada ya hapo toa na ukande upya kisha tengeneza katika shape za biskuti unazozipenda. Weka katika baking sheet kwa wanaotumia oven – weka katika oven biskuti zako – usiwe mbali na jiko kwani ndani ya dakika 15 – 20 zinatakuwa tayari pale utakapoona zinaanza kuwa brown katika kona na biskuti.
  4. Zikiwa tayari wazitoa na kuacha zipoe kwa dakika 5 basi hapo zipo tayari

KWA WATAKAO TUMIA MKAA

Uwe na sufuria kubwa alafu punguza mkaa kabisa katika jiko ikiwezekana acha kijikaa kimoja kidogo sawa – panga biskuti zako katika sufuri weka jikoni kisha funika na palililia mkaa mwingine kwa juu. Uwe makini sana kwa hii kwani ni rahisi kuunguza – ila ukipatia ni njia rahisi sana pia. Uwe unafunua kuchungulia kila baada ya dakika 5.
Waka

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *