Jinsi ya Kutengeneza Chocolate Moto | Hot Chocolate

7 Likes Comment

Hii ni ile wanaita Hot Chocolate; kusema kweli sijajua katika lugha ya kiswahili inaitwaje ila nimeona niite tu Chocolate moto ): . Ni rahisi sana namna ya kuiandaa na mahitaji yanapatikana kirahisi pia.

MAHITAJI

  • Cocoa 100 gm
  • Sukari laini kama ile ya keki 70 gm
  • Chumvi laini kijiko 1 cha chai
  • Udaha 1/4 kijiko cha chai ( Hiyari)

JINSI YA KUTENGENEZA

  1. Hatua moja tu – changanya vyote kwa pamoja. Kisha hifadhi kwenye chombo kikavu kama kopo la glasi na lenye mfuniko. Matumizi yake ni kila unapohitaji.

Kupata kikombe cha Chocolate moto – Chemsha full cream milk. Katika Kikombe weka vijiko viwili au kwa kadiri upendavyo kisha mimina maziwa yako na ugoroge vema ila ichanganyike vema kinywaji chako kitakuwa tayari.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *