Jinsi ya Kuunga Maharage na Nazi | Kula na Wali Nazi

21 Likes Comment

Maharage ni mboga inayoliwa sana na inawapenzi wengi ingawa kuna wengi pia hawayapendi ni kwa vile waliyala sana sijui enzi zile kwa sisi tuliosomaga Boarding schools. Leo nimekuletea jinsi ya kupika maharage kwa nazi au niseme kuunga maharage kwa nazi kisha kula wali wa nazi pia.

MAHITAJI

  • Maharage 1/4
  • Vitunguu maji 2 – Menya katakata
  • Kitunguu swaumu na tangawizi kijiko 1 cha mezani
  • Tui la nazi moja
  • Chumvi kiasi upendacho
  • Pilipili kiasi upendacho ( hiyari)

JINSI YA KUPIKA

  1. Kwanza chemsha maharage hadi kuiva kabisa
  2. Sasa katika kikaangio chako weka mafuta ; yakipata moto weka vile vitunguu maji ila nusu. Kaanga kwa dakika mbili kisha weka ule mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi kisha endelea kivikaanga na ikiwa kama vinabadili rangi sasa weka maharage na vile vitunguu vilivyosalia.
  3. Unaweza kuongeza chumvi mda huu pia na weka maji kidogo yake yaliyotumika kuchemsha maharage. Wacha vichemke kwa dakika 4 hadi 6 .
  4. Sasa weka tui la nazi na endelea kukoroga taratibu ili tui lisikatite. Vitakapoanza kuchemka tena waweza acha kwa dakika 3 hivi na mboga yako ya maharage itakuwa tayari kwa kula.

Mimi nilikuwa na wali wa nazi pamoja na turmeric – ingia hapa kuona jinsi ya kuupika wali wa njano.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *