Mboga Mboga Roast | Nzuri Kula na Chapati

1 Like Comment

Pishi hili lingefaa sana kwama tungeita Vegetable roast. Ila kwa vile naandika kiswahili mie na nakosa majina ya kiswahili kwa mapishi baadhi. Hili la leo nimelipa jina la Mboga Mboga Roast. Upishi huu una asili ya uhindi wale wasiokula nyama.

MAHITAJI

 • Bamia 1/4 kg – katakata
 • Biringanya 1 – katakata
 • Vinguu maji 2 vikubwa – katakata
 • Kiazi mviringo 1 – katakata vipange vidogo vidogo
 • Mafuta ya kula mazuri ( Olive Oil) vijiko 3 vya mezani
 • Mahanjumati masala au mchanganyiko wowote wa viungo – kijiko kimoja cha chai
 • Binzari manjano kijiko 1 cha chai
 • Mchanganyiko wa Kitunguu swaumu na Tangawizi kijiko 1 cha mezani ( Garlic and Ginger Paster)
 • chumvi kwa kiasi upendacho
 • Pilipili kwa kiasi upendacho ( Hiyari)

JINSI YA KUPIKA

 1. Kwanza weka mafuta katika pan ( chombo unachotumia kupika) yakiwa yanapata moto weka vitunguu maji, vipike kwa dakika chache vilainike tu. Kisha weka mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi na endelea kuvipika kwa pamoja kwa dakika 2.
 2. Sasa weka viaziĀ  na weka na chumvi kidogo endelea kuvikaanga pamoja, Havitachukua muda sana kuiva maana umevikatakata vidogodogo
 3. Kama waona vinakauka au kushika chini waweza kuwa unongeza maji kidogo kidogo kwa kutumia kijiko
 4. Baada ya dakika kama 3 sasa weka Bamia na zipike kwa dakika 3 na uweke zile bilinganya zako
 5. Sasa weka viungo vyako vyote na chumvi kufikia kiasi upendacho kisha uendelee kupika; hadi pale vitakapokuwa vimelainika na kuiva

Baada ya kuiva mboga hii ni nzuri sana kula na chapati au wali.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *