Mchanganyiko wa Matunda na Kabechi

Like Comment

 

Matunda ni matamu sana kama yalivyo ila pia ukiyachanganya unapata kitu kitamu zaidi. Sasa katika mchanganyiko huu wa matunda kabechi inahusika kama ifuatavyo

Matunda mix kwa watu 2

MAHITAJI

  • Embe dodo 1 ( Menya na kulikata kata vipande vidogo vidogo)
  • Karoti 2 ( kwangu ganda la juu na kukata kata vipande vidogo vidogo)
  • Kabechi 1/4 (Kata ndogo ndogo kisha loweka kwa maji moto kwa dakika 2 )
  • Tango 1 ( menya na kulikataka kata ila ondoa mbegu za ndani)
  • Maji ya limao vijiko vya 2 vya mezani
  • Parachichi 1 ( menya na kulikata kata)
  • Chumvi kidogo tu – au lah kwa kiasi upendacho

NAMNA YA KUCHANGANYA

  1. Ni rahisi sana changanya vyote katika bakuli au chombo kitoshacho. Na hapo ni tayari kwa kula. Ni mchanyanyiko mtamu sana

*MUHIMU*

  • Embe liwe limeiva vizuri
  • Parachichi liwe limeiva vizuri

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *