Mdizi Mzuzu ya Kuchoma na Jibini (Cheese)

1 Like Comment

 

Hili nipishi lingine dogo ila tamu na najua hapa kwetu Tanzania hatujazoea sana. Mimi huwa napenda sana kuchoma ndizi mzuzu na mara nyingi natumia jiko la oven. Sasa siku moja nikaongeza na jibini katika hizo ndizi; na kwa vile zilikuwa nzuri sana ndipo nikaamuka kuweka katika maandishi.

Ndizi za mtu 1

MAHITAJI

  • Ndizi mzuzu 2 ( zilizoiva kiasi)
  • Jibini ( Mozarella Cheese) kiasi kidogo
  • Giligilani fungu la kutosha mkono
  • Olive oil kijiko 1 cha mezani
  • Chumvi 1/2 cha chai
  • Pilipili kidogo ( sio lazima)

JINSI Y AKUPIKA

  1. Pasha jiko lako moto kwa ajili ya kuchoma ndizi – Zimenye na kuzichoma. Zikiwa zinaiva ndio muda wa kuandaa salad yako ndogo
  2. Changanya giligilani iliyokatwa katwa, mafuta, chumvi na pilipili kisha ziweke kando
  3. Ndizi zikiwa zimeiva pasua katikati na weka ile jibini kisha rudisha katika moto kuruhusu ile jibini kuyeyuka kidogo.
  4. Baada ya kuyeyuka jibini toa katika moto na nyunyuzia hiyo salad na hapo ni tayari kwa kula ndizi tamu na zenye jibini. Furahia.

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *