Pishi la Bamia za Kukaanga – Bites

4 Likes 1 Comment

Kuna bites za aina mbali mbali ila ninazo zipenda mimi ni hizi za Bamia za kukaanga. Na napenda kuwashirikisha katika kile kilicho kizuri kabisa.

MAHITAJI

  • Bamia kiasi cha robo
  • Mafuta ya Kupiki kwa kuaanga ( deep Fry)
  • Chumvi kiasi upendacho
  • Udaha 1/2 kijiko cha chai
  • Pilipili Manga 1/2 kijiko cha chai

JINSI YA KUZIKAANGA

  1. Kwanza andaa mchanganyiko wa viungo vikavu yaani chumvi, pilipili manga na udaha.
  2. Kataka kata katika slices zile bamia
  3. Pasha mafuta katika kikaangio chako kufikia joto la juu kati ( medium high); weka bamia zako na uzikaange hadi zitakapoanza kubadirika rangi na kuwa khawia basi wazitoa na kuweka kwenye chombo kingine
  4. Kabla kazijapoa kabisa ndio wanyunyiza ule mchanganyiko wa chumvi, pilipili manga na udaha.

Baada ya hapo ni tayari kwa kula taratibu zikuwa zimepoa au za moto moto.

About the Author: Chef Kile

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *