Pishi la Supu ya Bamia Karoti na Yai la Kuchemsha

1 Like Comment

Kwa wale wasiopenda vitu vya kunenepesha basi ni vema sana kama watakuwa wanaitumia supu hii kama kifungua kinywa chao. Ni supu rahisi sana kuiandaa na wala haichukui muda

Pishi la mtu mmoja

MAHITAJI

 • Bamia mbichi na changa 1/4 kg
 • Karoti moja
 • Yai moja – Lichemshwe
 • Kitunguu maji kimoja kidogo – Kilicho katwa katwa
 • Punje moja ya Kitunguu swaumu – kilicho katwa katwa
 • Chumvi kwa kiasi upendacho
 • Mafuta ya Butter / Olive oil kijiko kimoja cha mezani
 • Pilipili ( Hiyari)
 • Maji

JINSI YA KUICHEMSHA

 1. Weka vyote katika chombo cha kuchemsha isipokuwa yai na maji ya limao. Ongeza maji kiasi ya wastani kisha wacha vichemke kwa dakika 5
 2. Vikisha kuchemsha weka katika bakuli – kisha menya lile yai la kuchemsha na ulipasue katikati na kuweka katika hiyo supu
 3. Waweza nyunyiza maji ya limao na kuweka pilipili kama wewe ni mpenzi
 4. Hapo ipo tayari kwa kuliwa

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *