Supu ya Nyama ya Ng’ombe na Tambi

1 Like Comment

Pishi hili rahisi na tamu sana, ni supu tu ila waiwekea na tambi za Spaghetti na inakuwa nzuri sana.

MAHITAJI

 • Nyama ya Ng’ombe – kata vipande vidogo dogo – 1/2
 • Chumvi kiasi upendacho
 • Kitunguu maji 1 – kikate kate
 • Punje 3 za kutunguu swaumu – katakata
 • Mchanganyiko wa viungi vya majani kijiko kimoja
 • Udaha kijiki kimoja cha chai
 • Majani fresh ya Giligilani
 • Tambi 200 grams
 • Pilipili mannga ( Hiyari)
 • Cheese / Jibini (Hiyari)

JINSI YA KUPIKA

 1. Kwanza chemsha nyama yako vizuri ikaiva – katika kuichemsha weka chumvi kidogo. Ikiisha kuiva weka kando.
 2. Chemsha maji kisha ongeza chumvi kidogo weka zile tambi zako nazi zechemke kwa dakika 8 au hadi pale zitakapokuwa zimeiva.
 3. Sasa rudishia ile nyama katika moto kama waona supu ni ndogo ongeza maji na pia kwa sasa weka kitunguu maji, kitunguu swaumu, udaha, mchanganyiko wa majani na pilipili manga – acha vichemke kidogo kisha weka tambi zako nazo zichemke kwa dakika 2 au 3.
 4. Pakua katika bakuli ulipendalo kisha weka na yale majani mabichi ya giligilani kwa harufu nzuri na kupendezesha chakula chako

Asante na furahia pishi lako .

You might like

About the Author: Chef Kile

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *