Vichapati Aina ya Taco

Like 3 Comments

Vijapati hivi ni vile ambavyo kule kwa wenzetu Mexico vinaitwa Puffy Tacos. NI virahisi sana kuviandaa na hutumia unga wa mahindi yaweza kuwa sembe au wa dona.

MAHITAJI

  • Unga wa mahindi 1/4 kg
  • Chumvi kiasi upendacho
  • Maji
  • Mafuta ya kukaangia

JINSI YA KUVIANDAA NA KUPIKA

  1. Changanya unga na chumvi kisha weka maji kidogo kidogo upate ugumu kiasi lakini yenye ulaini.
  2. Uwache unga huo kwa dakika 10 – 20
  3. Katika kuzipika pasha mafuta katika joto la juu kati.
  4. Tengeneza vigoroli vya unga huo kiasi kisha chezesha kwa kupiga piga kupata upo la kichapat kidogo kisha tumbukiza katika mafuta – zikiwa zinavimba basi wageuza acha kwa dakika chache vikibadirika rangi na kuwa Khahawia basi viko tayari toa na weka kwenye chombo ili kuchucha mafuta

Taco hufaa kula na kachumbali aina ya Guacamole , au mboga nyingine yoyote uipendayo.

You might like

About the Author: Chef Kile

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *